Ukopaji wa msamiati ndio athari inayojitokeza zaidi katika lugha zilizoingiliana kuliko athari nyingine yoyote. Uchanganyaji wa lugha kwa maana ya kubadilisha msimbo ni matokeo ya muingiliano wa lugha. Muingiliano wa lugha husababisha muathiriano katika lugha, unaojidhihirisha katika ukopaji wa maneno, athari katika fonolojia, mofolojia sintaksia kwa maana ya mpangilio ya sentensi. Kwanza kabisa Kiswahili kiliingiliana na lugha ya Kiarabu, katika karne ya 12 wakati Waarabu walipoingia nchini kwa madhumuni ya kuendesha biashara.Baadae ikaingiliana na lugha ya Kijerumani na hatimaye lugha ya Kiingereza katika karne ya 19. Vilevile lugha huingiliana pale mtu anapotumia lugha mbili au moja baada ya nyingine, kwa maana ya kuchanganya lugha.Historia ya kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili inaonyesha kuwa, lugha ya Kiswahili imeingilina na lugha nyingi. Watu ambao ndio watumiaji wa lugha wamesababisha lugha kuiingiliana waliposafiri au kuhama sehemu moja hadi nyingine kutokana na sababu za kiuchumi, kijamii kiutamaduni na kisiasa. ![]() Kuingiliana kwa lugha sio jambo jipya katika dunia. ![]() Kuingiliana kwa lugha ni taaluma katika uwanja wa isimu inayohusu lugha zinazoingiliana na kuathiriana.
0 Comments
Leave a Reply. |